Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (MOEST), imeanza rasmi ujenzi wa jengo la ghorofa tatu katika chuo cha Ufundi Arusha lenye thamani ya shilingi, Bilioni 6.8.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi eneo ambalo jengo hilo linajengwa, Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi nchini(TVET), Mhandisi Thomas Katebalirwe, asema jengo hilo litasadia kuongeza idadi ya wanafunzi chuoni pamoja na kukidhi hitaji la Serikali la Wataalumu katika ujenzi wa Uchumi wa viwanda nchini.