MAELEZO YA MASOMO YA KUJIENDELEZA KWA MWAKA WA MASOMO 2019

Chuo kinatoa mafunzo kwa wale wanaotaka kufanya mitihani ya National Vocational Awards I (NVA I) katika fani za Biashara (Business Administration) Magari, Umeme wa Magari, Umeme, Electroniki, na Ujenzi. Mafunzo haya yanatolewa kwa makundi yafuatayo: a) Vijana waliomaliza Kidato cha nne (Form Four) na kupata cheti cha kidato cha nne cha Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) b) Wafanyakazi viwandani wenye ari ya kujiendeleza

A.    ORODHA YA KOZI (FANI) ZINAZOTOLEWA

Vijana wanayo nafasi ya kujiendeleza katika mojawapo ya kozi (fani) zifuatazo:

VOCATIONAL EDUCATION AND TRAINING (VET) COURSES

SN.

IDARA

FANI

CODES

SIFA

1

MAABARA

a)      Laboratory Technology NVA I-III

380

Kidato cha Nne (Form Four) na kupata cheti cha kidato cha nne (Certificate of Secondary Education Examination -CSEE) cha Baraza la Mitihani la Taifa

2

MAGARI

a)      Motor Vehicle Mechanics NVA I-III

570

Kidato cha Nne (Form Four) na kupata cheti cha kidato cha nne (Certificate of Secondary Education Examination -CSEE) cha Baraza la Mitihani la Taifa

b)      Auto Electrical- NVA I -III

630

3

UMEME

a)      Hydro Power Maintenance NVA I

Kidato cha Nne (Form Four) na kupata cheti cha kidato cha nne (Certificate of Secondary Education Examination -CSEE) cha Baraza la Mitihani la Taifa

b)      Domestic Electrical Installation NVA I-III

150

Kidato cha Nne (Form Four) na kupata cheti cha kidato cha nne (Certificate of Secondary Education Examination -CSEE) cha Baraza la Mitihani la Taifa

c)      Electronics – NVA I-II

180

d)     Refrigeration and Air Conditioning NVA I

170

e)      Industrial Electrical Installation NVA I

160

f)       Armature and Motor Rewinding  NVA I

190

4

MITAMBO

a)      Fitter Mechanics   NVA I-II

420

Kidato cha Nne (Form Four) na kupata cheti cha kidato cha nne (Certificate of Secondary Education Examination -CSEE) cha Baraza la Mitihani la Taifa

b)      Welding & Fabrication.-NVA I-II

440

5

MADINI

a)      Jewelry NVA I

990

Kidato cha Nne (Form Four) na kupata cheti cha kidato cha nne (Certificate of Secondary Education Examination -CSEE) cha Baraza la Mitihani la Taifa

b)      Gem Cutting NVA I

980

                                                      6

UJENZI

a)      Masonry and Brick Laying NVA I-III

20

Kidato cha Nne (Form Four) na kupata cheti cha kidato cha nne (Certificate of Secondary Education Examination -CSEE) cha Baraza la Mitihani la Taifa

b)      Plumbing and Pipe Fitting-NVA I-III

70

c)      Civil Drafting NVA I-II

60

d)     Road Maintenance NVA I

10

e)      Carpentry and Joinery NVA I

40

f)       Civil and Irrigation Practices (Prospective)

7

ICT

a)      Computer Applications NVA I

250

Kidato cha Nne (Form Four) na kupata cheti cha kidato cha nne (Certificate of Secondary Education Examination -CSEE) cha Baraza la Mitihani la Taifa

b)      Computer Maintenance NVA I

260

c)      Information Technology NVA I-II

270

8

TOURISM

a)      Tour Guiding NVAI

901

Kidato cha Nne (Form Four) na kupata cheti cha kidato cha nne (Certificate of Secondary Education Examination -CSEE) cha Baraza la Mitihani la Taifa

Kila mwombaji anatakiwa kuchagua “kozi/fani” moja tu kwa mwaka. Ili kupata waombaji wenye sifa zinazotakiwa pia katika kila fani kutakuwa na usaili (interview) kwa waombaji wote tarehe 07/01/2019.

Baada ya masomo ya mwaka wa kwanza (NVA I) mwanafunzi atakayefuzu mitihani ataruhusiwa kuendela na mwaka wa pili (NVA II) kwa kujaza fomu ya maombi upya. Atachaguliwa tu kuendelea iwapo katika mwaka wa kwanza na wa pili wa masomo alifuata ipasavyo masharti ya Chuo cha Ufundi Arusha.

Waombaji wanatakiwa wakati wa asubuhi wawe na sehemu ya kufanya mazoezi ya ufundi viwandani au katika karakana zinazohusiana na fani wanayoomba, ili waweze kuzingatia vizuri masomo watakayopata wakati wa jioni.

B.     KUENDELEA NA ELIMU YA JUU

Wanafunzi watakaoendelea mpaka kufanikiwa kupata  NVA III na kuwa na cheti cha kidato cha nne cha baraza la mitihani wataweza kupata nafasi ya kuendelea na chuo kwa masomo ya stashahada ya uhandisi katika moja ya fani zifuatazo:

a)      Stashahada ya Uhandisi Umeme (Diploma in Electrical Engineering)

b)      Stashahada ya Uhandisi Ujenzi (Diploma in Civil Engineering)

c)      Stashahada ya Uhandisi Mitambo (Diploma in Mechanical Engineering)

d)     Stashahada ya Uhandisi Mawasiliano (Diploma in Telecommunication Engineering)

e)      Stashahada ya Uhandisi Usafirishaji (Diploma in Transportation Engineering)

f)       Stashahada ya Sayansi na Teknolojia ya Maabara

g)      Stashahada ya Uhandisi Computer (Diploma in ICT/Diploma in Computer Science)

h)      Stashahada ya Uhandisi Magari (Diploma in Automotive Engineering, Auto Electrical and Electronic Engineering)

C.    MAMBO YA KUZINGATIA KWA WAOMBAJI

Kila mwombaji azingatie mambo yafuatayo:

1.      Gharama ya fomu ambayo HAITARUDISHWA ni shilingi Elfu Ishirini za Tanzania tu (20,000/=). (HATUPOKEI PESA TASLIMU). Wakati wa kufanya malipo ya fomu fika ofisi ya uhasibu Chuo cha Ufundi Arusha ili kupata Control Namba. Au tuma ujumbe kwenye namba hii 0762042717 ili kupata Control namba na namba ya account ya kulipia. Ujumbe huo uwe na taarifa zifuatazo. TAFADHALI USIPIGE SIMU.

a)      Majina kamili ya mwombaji

b)     Namba ya simu

c)      Ada ya maombi

d)     Kiasi (20,000/=)

Kumbuka kwamba ada ikishalipwa haitarudishwa kwa sababu yoyote ile.

2.      Fomu ya maombi irudishwe Ofisi ya Masomo ya Endelevu kabla ya tarehe 04/01/2019 pamoja na (passport size) mbili na ankara ya malipo ya benki (Pay in- slip)

3.      Fomu zitakazorudishwa baada ya tarehe hiyo hazitapokelewa.

4.      Usaili (interview) utafanyika tarehe 07/01/2019 saa 2.30 asubuhi hadi saa 08.00 mchana.

5.      Watakaofaulu usaili watapewa barua ya kuchaguliwa kujiunga na masomo

6.      Masomo yataanza rasmi tarehe 14/01/2019

7.      Mwombaji ahakikishe majina yaliyotumika katika cheti cha kidato cha nne (F.IV) ndiyo yatumike kujaza fomu hii ya maombi.

NB:-

Chuo hakitoi huduma za chakula wala malazi, mwanafunzi anatakiwa kujitegemea kwa hayo. Masomo ya Endelevu hutolewa siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 7:30 mchana mpaka saa12.30 jioni na Jumamosi kuanzia saa 2:30 asubuhi mpaka saa7.00 mchana.

Elimu Haina Mwisho

ZINGATIA

1.      Uje na kivuli (photocopy) ya cheti cha kuzaliwa au cheti cha uraia.

2.      Cheti (Certificate) au matokeo (Results slip) ya matokeo ya mitihani ya kidato cha nne (CSEE) cha Baraza la Mitihani la Taifa-Tanzania (NECTA) Leaving Certificate.

Bofya Hapa kupakuwa form za kusajili. (VET PROGRAMMES REGISTRATION FORM – 2019)