Chuo cha ufundi arusha (atc) kinawatangazia kuwa:

                        1. Muhula wa kwanza (first semester) kwa mwaka wa masomo 2018/2019 utaanza rasmi jumatatu tarehe 24 septemba, 2018.

                        2. Wanafunzi wapya wa mwaka wa kwanza (nta level 4) 2018/2019 wanatakiwa kuripoti chuoni kama ifuatavyo:

                        a) wanafunzi wanaodhaminiwa na serikali (waliochaguliwa kupitia tamisemi) wataripoti jumapili tarehe 16 septemba, 2018 kuanzia saa kumi kamili jioni

                        b) wanafunzi wanaojidhamini (private sponsored students) wataripoti jumatatu tarehe 17 septemba, 2018 kuanzia saa mbili kamili asubuhi.

                        3. Wanafunzi wanaondelea na masomo (nta level 5 & 6) kwa mwaka wa masomo 2018/2019 wanatakiwa kuripoti chuoni jumatatu tarehe 24 septemba, 2018.

                        4. Mambo yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa na wanafunzi wote:

                        a) mwisho wa kujisajili ni jumapili tarehe 07 oktoba, 2018 kulingana kanuni za usajili za chuo.

                        b) mwanafunzi ambaye atakuwa hajakamilisha usajili kufikia jumapili tarehe 07 oktoba, 2018 atapaswa kuomba upya nafasi ya masomo kwa mwaka 2019/2020. Maombi hayo yatapaswa kuzingatia miongozo itakayotolewa na nacte kwa mwaka husika.

               c) mwanafunzi ambaye hatakua amejisajili kwenye mfumo wa usajili wa chuo (atc online registration system) baada ya jumapili tarehe 07 oktoba, 2018 hataruhusiwa kuahirisha masomo kwa mujibu wa kanuni za usajili za chuo.

                        d) mwanafunzi aliyesajiliwa ni yule aliyelipa gharama za mafunzo kwa mujibu wa sheria za usajili za chuo

 

Imetolewa na ofisi ya usajili,

Chuo cha ufundi arusha.

13 septemba, 2018