Chuo kinapenda kuwatangazia kuwa kimepokea kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI Majina ya wanafunzi  waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya Stashahada katika Fani mbalimbali za ufundi zinazotolewa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) kwa mwaka wa masomo 2018/2019. 

 

Baraza la Taifa Elimu ya Ufundi (NACTE) limekiagiza Chuo kuwafahamisha kuwa kwa mwanafunzi aliyechaguliwa kujiunga na mafunzo ya Stashahada anapaswa kufanya UTHIBITISHO wa kukubali kujiunga na kozi aliyopangiwa kwa njia ya mtandao kuanzia tarehe 17 Juni, 2018 hadi ifikapo tarehe 8 Agosti, 2018. Tembelea tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz) katika kiunganishi (limnks) kinachoitwa Uthibitisho OR-TAMISEMI. Vile vile fomu za kujiunga chuoni zinapatikana kwa kupitia kiunganishi hicho. Hakikisha baada ya Uthibitisho kupitia NACTE unapakua Joining Instructions ya Chuo cha Ufundi Arusha.

 

Kwa wale wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kozi ya “Transportation Engineering” mnataarifiwa kuwa kozi hiyo kwa sasa imebadilishwa jina na inatambulika kama “Civil and Highway Engineering”.

 

KARIBUNI SANA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA; CHUO PEKEE NCHINI KINACHOTOA MAFUNZO YA ELIMU YA UFUNDI  ITAKAYOKUPATIA AJIRA KATIKA SOKO LA AJIRA

 

 

Imetolewa na OFisi ya Msajili wa Wanafunzi,

CHUO CHA UFUNDI ARUSHA