ELCT Press Release

Date: January 5, 2018
Press release No. 002/01/2018


Mkurugenzi wa Zamani wa Radio Sauti ya Injili aitwa mbinguni
(English below)


Marehemu Calvin Lyaro

Mkurugenzi wa zamani wa Radio Sauti ya Injili, Bw. Calvin Kimangano Lyaro, aliyeitwa mbinguni 06 Januari mwaka huu baada ya kuugua ugonjwa wa saratani kwa muda mrefu, amezikwa nyumbani kwake katika Kijiji cha Rau, Wilaya ya Moshi vijijini tarehe 11 Januari 2018.

Marehemu Lyaro aliyezaliwa 1942 alifanya kazi Radio Sauti ya Injili tangu 1967 hadi 2010. Ametumika katika ngazi ya Ukurugenzi kati ya 1995 hadi alipostaafu mwaka 2010.

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Jamhuri ya Watu wa Kongo lilianzishwa baada ya viongozi wake kusafiri toka Kinshasa hadi Moshi kwa kuwa wamevutiwa na mafundisho ya Neno la Mungu kupitia Radio Sauti ya Injili ambayo ilikuwa ikisikika Afrika Mashariki na Afrika ya Kati.

Imetolewa na:
Ofisi ya Katibu Mkuu, KKKT.


Former Director of Radio voice of the Gospel laid to rest

The former Director of Radio Voice of the Gospel (RVOG), Mr. Calvin Kimangano Lyaro, who passed on January 6, this year after a long battle with Cancer, was buried at his home in Rau village, Moshi Rural District on 11 January 2018.

The late Lyaro born in 1942 joined RVOG in Moshi, Northern Tanzania between 1967 and 2010. He served at the level of Director from 1995 until his retirement in 2010.

The Evangelical Lutheran Church in the Democratic Republic of the Congo (DRC) was established when its leaders travelled all the way from Kinshasa to Moshi to find out how they could join the Evangelical Lutheran Church in Tanzania (ELCT) because the teaching of the word of God broadcast by RVOG had bee reaching Eastern and Central Africa.

Issued by the:
Office of the Secretary General, ELCT.


Eric Adolf
Communication Coordinator,
Evangelical Lutheran Church in Tanzania
Box 3033, ARUSHA, Tanzania.
Phone: +255-27-250-8856/7
FAX: +255-27-254-8858
E-mail: erickin@elct.or.tz

For more information contact:

Eric Adolf
Communication Desk Officer, ELCT
E-mail: erickin@elct.or.tz