ELCT Press Release

Date: November 21, 2018
Press release No. 001/11/2018


Kanisa kuwa mwenyeji wa mkutano wa mabalozi wa elimu

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) litakuwa mwenyeji wa mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Mabalozi wa Elimu utakaofanyika Arusha kuanzia tarehe 22 – 25 Novemba 2018. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu Mkuu wa KKKT, Bw. Brighton Killewa, imesema kwamba mkutano huo ni sehemu ya kumbukumbu ya miaka 500 ya matengenezo ya Kanisa.

Mkutano huo wa mabalozi wa elimu umeandaliwa na Jumuiya ya Makanisa ya Kiinjili Ujerumani (EKD) ili kujenga mtandao wa Shule za Msingi, Sekondari , vyuo vya Ualimu pamoja vyuo vya juu vipatavyo 500 duniani kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu na kutumia zaidi mawasiliano kusaidi amani katika utoaji elimu. Kauli mbiu ya mkutano ni Mchango wa Mawasiliano katika kuinua ubora na amani katika utoaji elimu (Communication as a Contribution to Educational Quality and Peace Education).

Mkutano huo utawakutanisha wadau wa elimu wapatao 75. Kutoka nje ya nchi watakaoshiriki mkutano huo ni 61 na wengine ni kutoka Tanzania. Washiriki wa Tanzania ni pamoja na waratibu wa elimu kutoka Jumuiya ya Makanisa Tanzania (CCT) na wa Makanisa yaliyo chini ya CCT yaani Moravian, Presbyterian, Anglikana, Baptisti, Mennonites na KKKT. Wengine ni wawakilishi wa vituo vya elimu, shule na vyuo kutoka KKKT.

Aidha washiriki wa mkutano ni kutoka nchi zifuatazo: Rwanda, Jamhuri ya Watu wa Kongo, Cameroun, Sudani ya Kusini, Zambia, Madagacar, Zimbabwe, Ujerumani, Uholanzi, Ufaranca, Uingereza, Poland, Brazil, Argentina, Bolivia, Haiti, Hong Kong, Ufilipino, Marekani na Tanzania.

EKD (Evangelische Kirche in Deutschland) jumuiya ya makanisa 20 ya Kilutheri, Reformed (Calvinist) na Muungano wa Makanisa ya Kiprotestanti katika majimbo na madhehebu Ujerumani ambayo inawaunganisha Waprotestanti wengi katika nchi hiyo. EKD iliyoanzishwa 1945 ina makao yake makuu jijini Hanover.

Hadi sasa shule, vyuo na taasisi za elimu 732 zimesajiliwa kuwa wanachama wa mtandao wa GPENr hivyo kupita lengo la awali la kusajili shule vyuo na taasisi 500. Mkutano wa kwanza wa mabalozi wa elimu ulifanyika mwaka jana jijini Kigali, Rwanda.

ELCT hosts education ambassadors meeting

The Evangelical Lutheran Church in Tanzania (ELCT) will host the Second Education Ambassadors Assembly to take place in Arusha from 22 to 25 November 2018. A press statement issued by the ELCT Secretary General, Mr. Brighton Killewa, said that the gathering is one of the resolutions on Church reformation celebrations by churches in Germany.

The Ambassadors Conference on Education has been organized by the Evangelical Church in Germany (EKD) in order to establish a network of 500 primary schools, secondary schools, teachers and higher education colleges world-wide. The aim is use communication in order to improve the quality of education and instill peace through education delivery. The theme of the Ambassadors Conference is: “Communication as a Contribution to Educational Quality and Peace Education”.

The conference will bring together 75 education stakeholders out of which 61 delegates are foreigners while the rest are from Tanzania. Those from Tanzania include the educations coordinator of Christian Council of Tanzania (CCT) and representatives of schools under CCT including Moravian, Presbyterian, Anglican, Baptist, Mennonite and ELCT.

Participants of the conference come from Rwanda, DR Congo, Cameroun, South Sudan, Zambia, Madagascar, Zimbabwe, Germany, Netherlands, France, UK, Poland, Brazil, Argentina, Bolivia, Haiti, Hong Kong, Philippines, United States and Tanzania.

EKD (Evangelische Kirche in Deutschland) is a federation of 20 Lutheran, Reformed (Calvinist) and United (Prussian Union) Protestant regional churches and denominations in Germany, which collectively encompasses the vast majority of Protestants in that country. Founded in 1945, the EKD headquarters is in Hanover.

So far 732 schools, colleges and institutions have become members of GPENr network surpassing a 500 mark set earlier. The 1st Ambassadors conference was held last year in Kigali, Rwanda.


Eric Adolf
Communication Coordinator,
Evangelical Lutheran Church in Tanzania
Box 3033, ARUSHA, Tanzania.
Phone: +255-27-250-8856/7
FAX: +255-27-254-8858
E-mail: erickin@elct.or.tz

For more information contact:

Eric Adolf
Communication Desk Officer, ELCT
E-mail: erickin@elct.or.tz